Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A'rafi, Mkurugenzi wa Hawza za Elimu ya Dini nchini Iran, leo katika ujumbe wake, huku akitoa mkono wa pole kwa maombolezo ya Imam Hussein (as), kwa shahada ya Imam Shahidi na mashahidi wengine wapendwa, na akitoa shukrani kwa mashujaa wa taifa kubwa la Iran, alisema: “Yaliyotokea katika vita hii ya tatu ya kulazimishwa lilikuwa ni tukio kubwa la kihistoria na simulizi kubwa la ustaarabu, ambalo liliumbwa na taifa la Iran pamoja na mhimili wa Muqawama.”
Mkurugenzi wa Hawza aliendelea kusema: “Vipengele vya Muqawama, medani ya mapambano, juhudi za vikosi vya ulinzi na mhimili wa Muqawama, vyote vilikuwa nguzo muhimu sana. Hata hivyo, injini iliyochochea yote, moyo uliozalisha nguvu na nguvu kuu ya ushindi huu, ni ninyi wananchi wakubwa na wenye heshima mlioiumba hamasa hii adhimu.”
Kamilisheni Jihadi Yenu
Mjumbe wa Mafaqihi wa Baraza la Walinzi wa Katiba alisisitiza: “Mlolongo huu wa ushiriki wenu, jihadi hii kubwa, pamoja na msururu wa mawakibu na uwepo wenu barabarani, leo utaunganishwa na kiungo cha kuikamilisha ambacho kitakuwa dhamana ya ustawi na maendeleo ya nchi. Kiungo hicho ni kushiriki katika hafla ya mazishi na kuaga Imam wetu Shahidi, kufanya upya ahadi kwa Wilayat al-Faqih na kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kutangaza tena mshikamano wa kitaifa, na kukamilisha mlolongo huu wa ushiriki.”
Umuhimu wa Kushiriki kwa Wingi, kwa Namna Itakayowavunja Moyo Maadui na Kuleta Umoja
Ayatullah A'rafi alisisitiza kwamba katika kumuaga Imam wao Shahidi, katika mazishi ya mwili wake mtukufu, na katika hafla zote zitakazofanyika baada ya hapo, ni lazima yale yote yaliyofikiwa katika kipindi hiki cha miezi minne yakamilishwe kwa ushiriki mkubwa, wa kuvutia, wa kuwavunja moyo maadui na wa kuimarisha umoja wa taifa. Alisema hayo ndiyo matarajio yaliyopo kwa wanazuoni wa dini, wasomi wa vyuo vikuu, vijana wapendwa, pamoja na wanaume na wanawake wenye ghaira na ushujaa.
Mwishoni, Mkurugenzi wa Hawza alieleza matumaini yake kwamba, kwa hamasa na shauku ya taifa pendwa na lenye kujivunia la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, dunia itashuhudia hamasa mpya, simulizi jipya la kishujaa, na kuimarika zaidi kwa mnyororo wa Muqawama nchini Iran na katika eneo lote, kuanzia Lebanon, Iraq, Yemen hadi mataifa mengine ya Kiislamu.
Maoni yako